Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Marais wa China na Urusi katika taarifa ya pamoja, wakirejelea uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, walitangaza kwamba; “wanaafikiana kuwa mashambulizi haya ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na misingi ya mahusiano ya kimataifa, na kwamba yanadhoofisha kwa kiwango kikubwa uthabiti wa Mashariki ya Kati.”
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi, Moscow na Beijing zimesisitiza umuhimu wa pande zinazohusika katika vita kurejea haraka iwezekanavyo kwenye mazungumzo na majadiliano kwa lengo la kuzuia kuenea kwa mgogoro huo nje ya mipaka ya eneo hili.
Pia walitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua msimamo wa haki na usioegemea upande wowote, kusaidia kupunguza mvutano katika eneo la Asia Magharibi, na kwa pamoja kulinda misingi ya msingi ya mahusiano ya kimataifa.
Hapo awali, Xi alimwambia Putin kwamba hali ya Mashariki ya Kati ipo katika hatua nyeti na yenye maamuzi makubwa, Rais wa China alisisitiza kuwa; uhasama unapaswa kusitishwa mara moja, na akaashiria kuanzishwa upya kwa vita dhidi ya Iran kuwa jambo lisilokubalika.
Xi pia alieleza kwamba; kusitishwa vita kwa haraka kutasaidia kupunguza vikwazo vinavyoikabili sekta ya usambazaji wa nishati na biashara ya kimataifa.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, siku chache baada ya ziara ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani Donald Trump mjini Beijing, aliwasili katika mji mkuu wa China, mkutano wake wa pande mbili na Xi Jinping pamoja na mkutano mpana zaidi uliowahusisha wajumbe wa nchi hizo mbili ulifanyika, mwishoni mwa mikutano hiyo, nyaraka kadhaa, ikiwemo hati ya kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya pande hizo mbili, zilisainiwa.
Maoni yako